×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC SENDINGA AKABIDHI EKARI 8 KWA TAASISI YA MWINYI BARAKA ISLAMIC FOUNDATION

Na Mwandishi wetu.

MKUU wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendinga ameikabidhi Taasisi ya Mwinyi Baraka Islamic Foundation eneo la ekari 8 lililopo eneo la Makatanini Kata ya Maisaka Wilayani Babati Mkoani Manyara kwaajili ya ujenzi wa Msikiti, chuo cha mafunzo pamoja na huduma nyingine zote za kiimani na kijamii.

Akiongea mara baada ya kukabidhi eneo hilo Novemba 4, 2024 , Rc Sendinga amesema eneo hilo litumike kwa kusudi lililokusudiwa kwani litasaidia kukuza jamii kiimani pamoja na kuwainua vijana wengi kwenye fani mbalimbali zitakazowawezesha kupata kipato na kujiajiri.

Aidha RC Sendinga ametoa wito kwa wazawa wote pamoja na wegeni ndani ya eneo hilo kuwekeza kwenye Sekta mbalimbali zilizopo mkoani humo na watapatiwa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi na hatimaye waweze kufanikisha uwekezaji wao.

#NTTupdates