Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela, amefika katika Hospitali ya San Pio iliyopo Bukombe, kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya radi iliyotokea jana kwenye shule ya sekondari Businda wakati wanafunzi wakiwa darasani.
Ajali hiyo ilitokea jana Januari 27 2025 na kujeruhi wanafunzi ambao walikuwa wakiendelea na masomo, huku ikisababisha vifo vya wanafunzi saba.Mkuu wa Mkoa Shigela amesema kuwa ameguswa na tukio hilo ambalo limeacha vilio na simanzi kwa wananchi wa Bukombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amewasihi wanafunzi waliokumbana na kadhia hiyo kuendelea kuwa na subira na matumaini, akisema kuwa serikali itahakikisha inatoa msaada wa kila aina ili kuharakisha uponaji wa majeruhi.
Endelea kufuatilia NTTupdates kwa taarifa zaidi kuhusu tukio hili.
#NTTupdates.