Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Chelsea imemtoa kwa mkopo mlinzi wa kati, Renato Palma Veiga (21), raia wa Ureno kwenda kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia ambayo ilikuwa ikisaka huduma ya mlinzi wa kati.
Veiga ambaye unauwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani ambapo anauwezo wa kucheza kama Kiungo mkabaji au mlinzi wa kushoto anaungana na Pierre Kalulu na Federico Gatti ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi.
Msimu huu akiwa Chelsea amecheza michezo 18, akifunga magoli 2 na kutoa assist 1 kwenye mashindano yote ambayo Chelsea wameshiriki.
#NTTupdates