×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RUNGU LA TPLB LATUA KWA HERY SASII, FADLU NA SIMBA SC

Na Mwandishi wetu.

Taarifa rasmi kutoka bodi ya ligi kuu tanzania bara (TPLB) kupitia kwa kamati ya uendeshaji wa bodi ya ligi kuu, imemfungia mwamuzi wa kati (refa), Hery Sasii kutoka Dar es Salaam kwa miezi 6 baada ya kushindwa kusimamia ipasavyo sheria 17 za mpira wa miguu kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Mnyama Simba SC dhidi ya Singida Black Stars.

Mwamuzi Hery Sasii alishindwa kabisa kumudu mchezo huo ambao Simba SC walishinda goli 1-0 huku Singida Black Stars ikipoteza alama 3 kwenye mchezo huo huku akikataa kuwapa penati tatu za upande wa upande wa Singida Black Stars.

Pia kamati ya hiyo imeitoza klabu ya Simba SC faini ya Milioni 5 baad aha mashabiki wa klabu hiyo kurusha chupa za maji uwanjani kwenye mchezo ambao uliwakitanisha Simba SC dhidi ya Singida Black StarsHuku Kocha mkuu wa Simba SC, Fadlu Davis ametozwa faini ya Milioni 2 kwa kosa la kuishutumu bodi ya ligi kuu (TPLB) kuwa ina ajenda tofauti kutokana na ratiba ya vipolo kwa timu hiyo.

#NTTupdates