Watu saba wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kuharibu miundombinu ya shirika la umeme nchini TANESCO na kukutwa na vifaa mbalimbali kama nyaya za shaba, Earth wire na winding za ndani ya transformer.
Aakizungumza na waandishi wa Habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema watu hao wamekamatwa kwenye msako maalum wa uliowahusisha maafisa wa TANESCO kanda ya ziwa pamoja na askari polisi mara baada ya kuwepo kwa taarifa ya uharibifu wa miundombinu ya serikali kwa kuiba nyaya za shaba zilizomo ndani ya transfoma kitendo ambacho ni kinyume na sheria.
Aidha kamanda Mutafungwa amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Karoli Clement, Daniel Magege, John Deogratius, Bahati Stanley, Marwa Dismas, Wilson Joseph, Ally Tarimo na kusema pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.