Na Mwandishi wetu.
Watu saba wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo hii, eneo la Kihanga Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imehusisha gari kubwa la mizigo aina ya Scania ambalo limeyagonga magari mengine mawili ya abiria yaliyokuwa yamesimama ambayo ni Hiace inayofanya safari zake kati ya Karagwe na Mutukula pamoja na Coaster inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Karagwe leo.
“Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari aina ya Scania ambaye alikua katika mwendo kasi na kuyagonga magari haya mawili yaliyokuwa na abiria ambayo yalisimama yakiwa yanakaguliwa na Maafisa kutoka Idara ya Uhamiaji kwenye barrier ya ukaguzi” Amesema Chatanda
RPC Chantanda amesema Katika vifo hivyo saba Wanawake wanne, Mwanaume mmoja na Watoto wawili, majeruhi Wanaumewanne na Wanawake watano, huku chanzo kikiwa ni uzembe wa Dereva.
#NTTUpdates