×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SAFARI ZA MABASI USIKU ZAPAMBA MOTO, 2323 YAPEWA KIBALI

Na Mwandishi wetu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu Suluo, amesema tangu kuanza kwa mfumo wa safari za saa 24 hadi kufikia Macho 31, Mwaka huu jumla ya Mabasi 2323 tayari yamepewa kibali Cha kutoa huduma ya safari hadi nyakati za Usiku.

CPA Suluo amesema yapo Mabasi mengi lakini sio yote ambayo yanaweza kusafiri usiku na Mchana na Basi likifanya safari usiku Mfumo wa LATRA unatoa taarifa kuwa gari haliruhusiwi kusafiri usiku.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano na Wahariri pamoja na Wanahabari kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari nchini, Leo April 14, Mwaka huu, Jijini Dar es salaam.

#NTTUpdates