Na Mwandishi wetu.
Mabingwa wa ligi kuu Morocco, Raja Athletic Club wamefanikiwa kumsajili winga wa timu ya Taifa ya Senegal Pape Ousmane Sakho (27) akitokea Guevilly ya nchini Ufaransa baada ya mkataba wake kutamatika.
Winga huyo ambae aliwahi kupita Simba SC na kushinda tuzo ya goli bora la mwaka kwenye michuano ya vilabu ya CAF 2022, atarejea tena kwenye michuano hiyo baada ya klabu hiyo kufuzu hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
#NTTupdates