Na Mwandishi wetu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema tasnia ya burudani ambayo michezo ipo ndani yake imeendelea kukua kwa kasi kubwa na kuchangia Pato la Taifa na kuongeza ajira nchini ambapo 2022/23 ilikua kwa asilimia 15 na mwaka 2023/24 kwa asilimia 18.
Biteko ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za serikali (SHIMIWI) kwa Mwaka 2025 katika uwanja wa CCM Kirumba wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.
amesema watumishi nchini ni sehemu ya kukua kwa sekta hiyo kupitia SHIMIWI kwani wamekua wakiwakusanya maelfu ya wachezaji katika kushindana na kujenga hari ya kimichuano wakati wote hivyo wamekua wakiichagiza jamii kuthamini michezo na kuruhusu hata vijana kushiriki.
Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameishukuru Serikali kwa kuufanya mkoa huo kuwa Kitovu cha Michezo kwa kuwekeza katika michezo ambapo inajenga Kituo cha Kulea Vipaji katika Chuo cha Michezo Malya kwa zaidi ya Bilioni 31.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamadini na Michezo Bw. Gerson Msigwa amesema kuwa mashindano hayo kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo hayajasimama na ameahidi wizara hiyo kuendelea kusimamia michezo hiyo ikiwa ni pamoja na kusimamia haki ili mshindi apatikane kihalali.
#NTTupdates.