×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SELEMAN MWALIMU MCHEZAJI BORA MWEZI SEPTEMBA

Na Mwandishi wetu.

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya Fountain Gate FC Seleman Mwalimu, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba 2024.

Seleman Mwalimu amewashinda wachezaji wenzie ambao ni mshambuliaji wa Fountain Gate FC William Edgar na kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salumu.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa MVP na mfungaji Bora msimu uliopita kwenye ligi kuu ya Visiwani Zanzibar pia ndiye kinara wa upachikaji mabao NBC msimu huu akiwa na magoli 5 kwenye michezo 7 ambayo mpaka sasa Fountain Gate FC imecheza.

#NTTupdates