×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WATUMISHI NCHINI

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Amir Mkalipa ameahidi kufikisha changamoto ya nyongeza ya mshahara kwa watumishi ambao tayari wameisha fikia ukomo wa vyeo kwa mamlaka husika ili ziendelee kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi wote.

Amesema hayo leo terehe 11 septemba, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa Kamati ya wanawake THTU Taifa 2025 ulioandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU).

Sambamba na hayo amempongeza balozi Getrude Mongella kwa mchango wake wa kusimamia harakati na mafanikio ya wanawake duniani kupitia mkutano wa Beijing.

“Niungane na nyie kumpongeza na kumshukuru mwanamke shupavu aliyeshiriki katika mapambano ya mafanikio kwa wanawake na pia tumepokea salamu zake kwenye mkutano huu” Amesema Mhe. Mkalipa.

Naye, Mwenyekiti wa THTU Taifa Dkt. Paul Loisulie amefafanua kuwa ni utaratibu wa chama hicho kukutanisha majukwaa katika nyakati tofauti ili kutoa fursa kwa kila kundi kupata nafasi ya kutathmini kazi zao kama chama cha wafanyakazi na kwamba lipo Jukwaa la vijana ambalo limekutana Morogoro kwa mwaka huu.

“Pamoja na majukumu mengine tunaketi pamoja kama wafanyakazi na kujadiliana dhana ya vyama vya wafanyakazi kama vyombo vya kushauri kwani vimekua havieleweki kwa walio wengi hususani kwa waajiri ambapo siku za nyuma walidhani chama kipo kwa ajili ya kufanya harakati”, amesema.

“Mwanamke akiwa na maarifa anakua na uwezo, ushawishi na ari ya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali na hata kujiusisha na siasa kwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu na kuweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi.” Amesema Bi. Roselyne Massam wakati akitoa risala kwa niaba ya washiriki.

Akisoma risala Mratibu msaidizi wa kamati ya wanawake THTU Bi. ameiomba serikali kutazama muongozo wa nyongeza ya mshahara kwa watumishi ambao tayari wameisha fikia ukomo wa vyeo na mshara.

#NTTupdates.