×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI YABORESHA HUDUMA ZA SARATANI YA MATITI KUPITIA MRADI WA PFIZER MWANZA

Na Mwandishi wetu.

Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Jhpiego imeendelea kuboresha huduma za matibabu ya saratani ya matiti Mkoani Mwanza kupitia Mradi wake wa PFIZER – Beat Breast Cancer awamu ya pili ambao unalenga kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa kuimarisha uchunguzi wa mapema na upatikanaji wa matibabu.

Akizungumza leo Oktoba 22, 2025 na waandishi wa habari ofisini kwake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Jesca Lebba ameipongeza serikali kwa hatua hiyo muhimu na kuishukuru kwa kuuchagua Mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa wanufaika wa awamu ya pili ya mradi huo.

Naye Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure Dkt. Jackson Chiwaligo amewasisitiza wanawake kujifanyia uchunguzi wa awali ili waweze kutambua mabadiliko katika miili yao, huku akitoa wito waweze kufika hospitali pale ambapo watahisi mabadiliko yoyote katika matiti.

#NTTupdates.