×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI YAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE MAFUNZO KWA WALIMU WAPYA

Na Mwandishi wetu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa walimu wapya ili kuwaandaa kufundisha katika shule mbalimbali nchini kwa ufanisi na weledi.

Akizungumza leo Mei 12, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Prof. Mkenda amesema hatua hiyo inalenga kuboresha kiwango cha elimu na kuinua ufaulu wa wanafunzi.

Ameeleza kuwa walimu wapya wanapewa mafunzo ya kina yanayolenga kuwajengea uwezo wa kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi na teknolojia ya kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na maarifa duniani.

Waziri Mkenda amesema Serikali imezidi kuimarisha usimamizi wa ubora wa elimu kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na yenye tija kwa maisha yao ya sasa na baadaye.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya shule, vifaa vya kufundishia na mazingira rafiki kwa walimu na wanafunzi ili kuhakikisha elimu inakuwa chombo cha ukombozi kwa kila Mtanzania.

#NTTupdates