×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SERIKALI YASISITIZA KUIMARISHA UTAFITI KATIKA SEKTA YA AFYA

Na Mwandishi wetu.

SERIKALI imesema itaendelea kuimarisha Mfumo wa Utafiti na kutumia matokeo,kutenga fedha za kufanyia tafiti na kusimamia tafiti lengo likiwa ni kuzidi kuiboresha sekta ya afya.

Hayo yameelezwa leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akifungua kongamano la Kisayansi katika kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Afya Kitaifa 2025.

Dk Shekalaghe amesema Utafiti wa magonjwa ya binadamu ni muhimu katika kuboresha huduma za afya na Kinga ambapo amedai Serikali itahakikisha inazitumia tafiti hizo.

“Miradi mingi ya Utafiti imetekelezwa na Serikali imefanya mambo makubwa kwa kusaidiwa na tafiti hizo ambapo dhamira ni kuimarisha tafiti kwa kutumia tafiti.”amesema Dkt.Shekalaghe

Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Dk Grace Maghembe amesema wameona hawawezi kuadhimisha wiki ya Afya bila kuwa na majadiliano ya kitaaluma.

Amesema forum hiyo imeleta wataalamu mbalimbali lengo ni kupata mawasilisho mbalimbali katika sekta ya afya,kubadiishana uzoefu na kuona namna gani ya kufanya vizuri zaidi.

Pia watapata Nafasi ya kujifunza kupitia wale ambao wanaofanya vizuri zaidi Amesema kupitia kauli mbiu tulipotoka tuendapo na tulipo katika sekta ya afya watajifunza mambo mbalimbali huku kwa upande wa tafiti wameweka wabobevu na wale wanaoelekea katika ubobovu.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Dk Rashid Mfaume amesema wanajivunia maboresho katika sekta ya afya kwa kuwezesha vituo vya Afya kundaa mipango yao wenyewe.

#NTTupdates