Na Mwandishi wetu.
Tamasha kubwa la soka la Klabu ya Simba SC maarufu kama Simba day msimu wa 2025/2026 limetangazwa rasmi kuwa litafanyika tarehe 10 Septemba 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.
Tamasha hilo ambalo ni kama Sikukuu ya mashabiki wa Simba SC hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa msimu mpya wa ligi kuu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wao kwa mashabiki wa klabu hiyo ambapo burudani mbalimbali zinakuwepo kuyanikiza Tamasha hilo na humalizika kwa kuchezwa mchezo wa kirafiki baina ya Simba SC dhidi ya Timu itakayoalikwa siku hiyo.
#NTTupdates.