Na Mwandishi wetu.
Uongozi wa Klabu ya Simba SC imetoa taarifa rasmi kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ikisisitiza kuwa mchezo namba184 dhidi ya watani wao Young Africans SC utapigwa Juni 15, 2025 kama bodi ya ligi walivyopanga na ikiwataka mashabiki wa klabu hiyo kujiandaa kwenda kuujaza Benjamin Mkapa, Dar es Salaam siku hiyo.
Pia imewataka bodi ya ligi kuu TPLB kutoa ripoti ya uchunguzi ili wale wote waliohusika na kile kilichotokea Machi 7, 2025 ambapo Simba SC walizuiliwa kuingia uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mazoezi ya mwisho na kupeleka vurugu wachukulie hatua za kisheria.
Kwenye taarifa yao Simba SC wameweka wazi kuwa kutochukuliwa hatua kwa wanaoendelea kuchochea ghasia ni sawa kulinda uharamia katika Mpira ambao unatia dosari mafanikio yaliyopo katika tasnia ya mpira wa miguu nchini kwa sasa.
#NTTupdates