
Dakika 90 zimemalizika katika dimba la CCM Kirumba jijini mwanza na kushuhudia wenyeji Pamba Jiji FC wakigawana alama moja dhidi ya Mnyama Simba SC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC baada ya mchezo kutamatika kwa share ya 1-1.
Simba SC ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa kiungo mshambuliaji wao Oura dakika ya 33 na baadae Pamba Jiji FC kupitia kwa Mwashinga dakika ya 35′ kupitia mpira wa adhabu.