×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

SIMBA SC YATISHIA KUSUSIA KARIAKOOO DERBY LEO

Na Mwandishi wetu.

Klabu ya Simba SC imetoa taarifa rasmi kupitia kurasa za mitandao yao ya kijamii kuwa hawatashiriki kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Young Africans SC maarufu kama Kariakoo Derby baada ya sintofahamu iliyojitokeza hapo jana kwenye dimba la Benjamin Mkapa baada ya kushindwa kufanya mazoezi ya mwisho walipozuiliwa na wanaodaiwa kuwa Makmandoo wa Young Africans SC.

“Siyo mechi ya kesho tu hatuchezi mechi ya ligi ya mpaka hawa wapuuzi walioshiriki kwenye huu upuuzi waadhibiwe”

Maneno hayo yameandikwa na Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC Crecentus Magori kupitia mtandao wake wa kijamii.

Mchezo wa Kariakoo Derby utapigwa leo majira ya saa 1:15 usiku kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam huku mashabiki wa timu zote mbili wakisubiria taarifa rasmi kutoka bodi ya ligi kuu (TPLB)

#NTTupdates