Na Mwandishi wetu.
Baada ya kushindwa kubeba ubingwa wa serie A na klabu ya Inter Milan ya Italia, Aliyewahi kuwa Kocha wa klabu hiyo Simone Inzaghi (49), ametambulishwa rasmi kuwa Kocha mkuu wa klabu ya Al Hilal.
Al Hilal SC inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia imempa mkataba wa Hadi 2027 kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Jorge Jesus ambaye ametimuliwa kwenye klabu hiyo.
Matajiri wa klabu ya Al Hilal wanaamini kocha huyo atarudisha makali ya klabu hiyo kama alivyofanya italia baada ya kuipeleka Inter Milan fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya UEFA) licha ya kupoteza mchezo huo mbele ya PSG ya Ufaransa.
#NTTupdates