Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Al Nasri SC ya Benghazi nchini Libya imekubali kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Jonathan Sowah (24) kujiunga na Singida Black Stars FC kwa dau la Dola za Marekani 220,000 (Milioni 585).
Mshambuliaji huyo ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika Disemba 2025 lakini Al Nasr SC, imekubali kumuuza mchezaji huyo ambaye alinunuliwa na klabu hiyo kutoka Medeama FC ya nchini kwao Ghana.
Sowah ambaye anatajwa kama mchezaji muhimu kwenye Kikosi Cha Medeama FC msimu wa 2022-2023 ambapo alicheza michezo 20 na kufunga magoli 12 na assist 1.
Pia aliwahi kuhusishwa kujiunga na Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania Young Africans SC baada ya klabu hiyo kumuuza mshambuliaji wao Fiston Mayele kwenda Pyramid lakini dili hilo lilishindikana na mshambuliaji huyo akatimkia Libya.
#NTTupdates