×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

STARS YACHAPIKA MOROCCO

Na Mwandishi wetu.

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imepoteza mchezo wake wa hatua ya makundi kuwania kufuzu michuano ya kombe la Dunia 2026, dhidi ya Morocco baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-0 na kuifanya Morocco kuwa Taifa la kwanza kutoka Afrika kufuzu michuano hiyo, ambayo yatafanyika kwenye mataifa matatu ya Marekani, Mexico na Canada.

Hadi dakika 45′ za kipindi cha kwanza zinamalizika Stars ilifanikiwa kuizuia safu ya ushambuliaji ya Morocco isipate goli la kutangulia lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili kupitia kwa Nayef Aguerd ambaye aliitanguliza Morocco dakika ya 51′ na Brahim Diaz dakika ya 58 kupitia mkwaju wa penati.

Stars ambayo imepangwa Kundi E na mataifa ya Morocco, Niger, Congo, Zambia na Eritrea italazimika kushinda michezo yake miwili iliyosalia, ambayo ni dhidi ya Zambia na Niger ili kupata nafasi ya kucheza Play off.

#NTTupdates