×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TANESCO YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI GESI ASILIA

Na Mwandishi wetu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Daktari Doto Biteko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Kuhakikisha linaongeza uzalishaji wa gesi hili kusaidia kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme hapa nchini.

Waziri Daktari Biteko ameyasema hayo jijini Dar-Es-Salaam wakati alipotembelea na kukagua Miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II pamoja na Kituo Cha kupokea gesi asilia kinyerezi ikiwa ni sehemu ya kukagua miundombinu ya usafirishaji gesi huku akibainisha kuwa yapo maboresho makubwa yamefaywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika kuwahudumia wananchi juu ya mahitaji ya hayo.

Aidha ameongeza kuwa upatikanaji wa umeme unaendana na mahitai ya ongezeko la watu na TANESCO inatarajia Kuongeza uzalishaji umeme katika Kituo Cha kinyerezi III kutoka megawati 600 katika mpango wa awali hadi kufikia megawati 1000 hili kusaidia upatikanaji mkubwa wa Umeme.

Amesema Kupitia mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) pekee uzalishaji kiwango Cha umeme Megawati 2115.

#NTTupdates