Na Mwandishi wetu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amesema ikiwa ni sehemu ya manufaa ya nchi kutokana na Mkutano wa Afrika wa Nishati unaoanza Dar es Salaam kesho Januari 27, 2025, Wizara ya Maliasili na Utalii imekamilisha kuweka vivutio mbalimbali vya utalii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumapili Januari 26, 2025 mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyowekwa vivutio hivyo na akiwa ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (Utalii), Nkoba Mabula, Mkurugenzi Mkuu wa TTB Ephraim Mafuru na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Tawa na maafisa wengi pia Wizara hiyo, Dkt. Abbasi amesema Wizara hiyo imeweka taswira zenye ngozi halisi za wanyama kuanzia Terminal 1, 2, 3, ukumbini na kwenye mizunguko ya Ocean Road na Agakhan kuvutia wageni.
“Tuko tayari pia pamoja na taasisi zetu na wadau kupeleka wageni kwenye vivutio mbalimbali, tayari mfano kuna maafisa waandamizi wa Benki ya Dunia wanataka kwenda Serengeti tunaratibu na tunakaribisha wengine wengi,” amesema Dkt Abbasi.
#NTTUpdates