Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na nchi ya Omani ya kufungua soko la ajira ambapo kupitia mkataba huo vijana wa Kitanzania wataweza kufanya kazi zenye staha nchini Omani wakati wa Omani wakija kufanya kazi nchini Tanzania.
Serikali ya Tanzania kupitia kwa katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, JAMAL KATUNDU amesema serikali imeingia mkataba wa kubadilishana fursa za ajira kwa vijana kati ya Tanzania na Omani ili kuleta nguvu kazi shindani, jamii yenye Maisha bora na kazi zenye staha.