×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TANZANIA NA RWANDA ZASAINI HATI ZA UIMARISHAJI MPAKA WA KIMATAIFA

Na Mwandishi wetu.

Nchi ya Tanzania na nchi ya Rwanda zimetia saini hati ya Makubaliano (MoU) ya Uimarishaji mpaka wa Kimataifa ambao ni sehemu ya makubaliano ya umoja wa Afrika(AU) kuwa ifikapo 2027 mipaka yote iwe imeimarishwa baina ya nchi hizo.

Makubaliano ya utiaji Saini yamefaywa kati ya Mkurugenzi wa upimaji wa ramani kutoka wizara ya ardhi, nyumba na manendeleo ya makazi , Hamdouny Mansour na kiongozi wa ujumbe wa Rwanda, Abel Buhungu mara baada ya kukamilika kwa Kikao cha Kamati ya Pamoja cha Wataalamu (JTC) kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika katika mji wa Ngara mkoa wa Kagera.

Ukaguzi wa mpaka ulianza katika eneo la mafiga matatu(Kasange) na kuelekea hadi mji wa Rusumo ili kubaini hali halisi ya mpaka, shughuli za kibanadamu, maendeleo yaliyofanyika na Yale yanayoendelea kufanywa na nchi hizo.

Mara Baada ya ukaguzi huo nchi hizo zilikubaliana kuendelea kushirikiana kuimarisha mpaka na maazimio yaliyofikiwa yatatekelezwa kama walivyokubaliana ili kuendelea kuimarisha Hali ya ulinzi na usalama baina ya nchi hizo mbili.

#NTTUpdates