Na Mwandishi wetu.
Profesa Mohamed Yakub Janabi wa Tanzania leo May 18/2025 amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika mpya katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Uchaguzi huu umefanyika baada ya kura ya Kamati ya Kanda ya Afrika ya WHO huko Geneva.
Tangazo hilo limetolewa na Dkt. Louise Mapleh Kpoto, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Liberia, ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho.
#NTTupdates