×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TAWA YAPONGEZWA NA KAMATI YA BUNGE

Na Mwandishi wetu.

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ya ujenzi wa barabara ya Km 30 uliyogharimu Shillingi million 256 pamoja na ujenzi wa bwawa uliyogharimu Shillingi million 125 ndani ya Hifadhi ya wanyamapori Makuyuni Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.

Kamati hiyo ipo Jijini Arusha ikiendelea na ziara yake ya kikazi ya siku mbili tangu jana Machi 13, 2025 ndani ya mkoa huo chini ya Mwenyekiti wake, Timotheo Mnzava ambaye ameonyeshwa kuridhishwa na mwendo wa miradi hiyo.

Mnzava ametoa wito kwa Menejimenti ya TAWA kuendelea kuitangaza vyema hifadhi hiyo ili malengo yaliyokusudiwa yatimie lakini pia kutatua migogoro ya mipaka na kujenga uhusiano bora kati ya jamii na hifadhi hiyo.

Aidha, amebainisha matamanio ya Kamati hiyo ni kuiona TAWA inaendelea kubuni na kuwa na vyanzo vingi vya mapato ili iweze kujiendesha bila ya kutegemea fedha kutoka Serikali kuu.

#NTTupdates.