×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

TCRA YATOA ELIMU YA MFUMO MPYA WA SOUND BROADCASTING KWA WADAU WA VYOMBO VYA HABARI

Na Mwandishi wetu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya Kaskazini imekutana na wadau wa vyombo vya habari, katika semina ya mafunzo kuhusu mabadiliko ya teknolojia kuelekea mfumo wa kidigital wa Sound Broadcasting (DSB), iliyofanyika jijini Arusha.

Semina hiyo imelenga kuwapa uelewa wa kina wadau hao kuhusu mfumo huo wa kisasa wa kurusha matangazo ya sauti, ambao unatajwa kuboresha usikivu, kupunguza gharama, na kuongeza fursa kwa vyombo vya habari kufikia hadhira kubwa kwa ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika kikao hicho leo Juni 19, 2025, Meneja wa TCRA Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Francis Mihayo, amevitaka vyombo vya habari vya ngazi ya wilaya vinavyotamani kuwa vya mkoa kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo kulipia ada ya masafa huku akibainisha vituo vitakavyokamilisha hatua hiyo vitapaswa kuwasiliana na mtoa huduma aliyesajiliwa ili kuunganishwa kwenye mfumo wa kidigitali kwa mujibu wa mwongozo wa TCRA.

Kwa upande wake, Mhandisi Kisaka kutoka TCRA Makao Makuu amesema mfumo wa DSB utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya utangazaji kwani mfumo huo si tu unaongeza ubora wa sauti, bali pia una uwezo wa kuonyesha jina la kipindi na mtangazaji moja kwa moja kwenye kifaa cha kusikilizia, hatua itakayoongeza uwazi na mvuto kwa wasikilizaji.

Aidha, safa moja ya mfumo huo ina uwezo wa kubeba hadi masafa 14 kwa wakati mmoja, hivyo kupanua wigo wa urushaji wa vipindi kwa gharama nafuu.

#NTTupdates.