Na Mwandishi wetu.
Mambo yameendelea kuwa mazito kati ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) na Mabingwa wa kihistoria wa Tanzania bara Young Africans SC baada ya klabu hiyo kupitia kwa Afisa habari wao Ally Shabani Kamwe kutoa taarifa kwa vyombo vya habari hapo jana kuwa klabu hiyo haijapewa zawadi yake ya fedha ambazo walitakiwa kupewa baada ya kubeba taji la CRDB msimu uliopita.
TFF imetoa taarifa rasmi kwa umma kuwa hawadaiwi fedha yoyote na klabu ya Young Africans SC bali wao ndio wanaidai klabu hiyo na kuwataka watume mtaalamu wao wa fedha kesho saa 4:00 asubuhi ili kuhakiki madeni hayo.
Pia TFF wameweka wazi kuwa Young Africans SC iliomba shirikisho kwa njian ya maandishi kuwa fedha hizo zitumiwe kwa ajili ya kulipa vibali vya wachezaji wa kigeni pamoja na madeni yao.
#NTTupdates