Na Mwandishi wetu.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Monduli Mukhsin Kassim kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Monduli Festo Kiswaga, ameipokea timu ya wataalamu wa sheria kutoka Samia Legal Aid Campaign ambayo imefika Wilayani humo leo Machi 29, 2025 kwaajili ya kuanza zoezi la utatuzi wa migogoro mbalimbali inayohitaji msaada wa kisheria kwa wananchi wa Wilaya hiyo.
Bw. Kassim katika mazungumzo,yake , mara baada ya kuipokea timu hiyo ya wataalamu wa sheria amewataka wananchi wa Wilaya ya Monduli kuwa mstari wa mbele kwa kuchangamkia fursa hiyo ya msaada wa kisheria ambayo itadumu kwa muda wa siku kumi (10) ndani ya Wilaya hiyo katika vijiji 30 vya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na kusema kuwa ujio wa Kampeni hiyo ndani ya Wilaya hiyo itasaidia sana kwani ni moja ya Wilaya zinazokabiliwa na migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kampeni hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Wakili Tunsubilege Boniface amesema kuwa timu hiyo imeanza kazi yake ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi leo na siku ya Machi 30, 2025 itafika Kata ya mto wa mbu kwaajili ya kuendelea na zoezi hilo hivyo wananchi kutoka maeneo hayo wajitokeze kwa wingi kwani ni bure kupatiwa huduma hiyo.
#NTTupdates.