Na Mwandishi wetu.
Nyota Cristiano Ronaldo ameiongoza timu yake ya Taifa ya Ureno kubeba taji la pili la UEFA Nation League baada ya kupata ushindi dhidi ya Hispania kwenye dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani.
Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya magoli 2-2 ambapo Hispania ilikuwa ya kwanza kufunga goli kupitia kwa Kiungo wao M. Zubimendi dakika ya 21, dakika 5 baadae Ureno waliweka mzani sawa kupitia kwa Mlinzi wa kushoto Nuno Mendes dakika ya 26′, Hispania walirejea tena kambani dakika ya 45′ kupitia kwa O. Oyarzabal na kipindi cha kwanza kumalizika kwa Hispania kuiongoza magoli 2-1.
Kipindi cha pili mshambuliaji Cristiano Ronaldo aliipatia Ureno goli la pili dakika ya 61′ na kupelekea dakika 90 kumalizika kwa sare ya 2-2 na mchezo huo kuamuliwa kwa mikwaju ya Penati ambapo Ureno ilipata ushindi wa Penati 5-3.
#NTTupdates