×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

USHIRIKIANO WA SEKTA BINAFSI NA UMMA KATIKA KUKUZA UCHUMI

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amefungua mkutano wa Baraza la biashara la Mkoa na kuhimiza ushirikiano baina ya sekta binafsi na umma ili kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo leo Machi 14, 2025 katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa,,

Mtanda amesema siri ya mafanikio ya ukuaji wa uchumi ni ushirikiano na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa pamoja na siyo kukimbilia sehemu zisizo na msaada.

“Ofisi ya mkuu wa mkoa ndiyo mahali mwafaka wa kufikisha kero au changamoto zinazotishia kukwamisha shughuli za kibiashara,msikimbilie kwenye vyombo vya habari huo siyo uamuzi sahihi,” Mtanda

Kuhusu uchumi wa Mkoa wa Mwanza ambao kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2020-23 Mkoa huo umechangia Tshs Trilioni 13.5,Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha Serikali imewekeza miradi ya kimkakati ya Tshs Trilioni 5.6 hivyo itakapokamilika uchumi utazidi kupiga hatua.

“Tuna miradi iliyo mbioni kukamilika ikiwemo Daraja la JP Magufuli, Meli mpya ya Mv Mwanza na upanuzi wa uwanja wa ndege,vyote hivyo vikikamilika wigo wa biashara kutoka nchi jirani utapanuka na kuongeza uchangiaji wa pato la Taifa, ambapo sasa Mwanza inachangia 7.2% ukiwa ni Mkoa wa pili baada ya Dar-e-s Salaam inayoongoza kwa kumchangia 17% “Mkuu wa Mkoa.

Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Baraza la biashara la Taifa Dr.Godwill Wanga ameipongeza Serikali kwa kwa kutoa fursa zaidi za uwekezaji kwa sekta binafsi hali ambayo imeifanya sekta hiyo kuzidi kupiga hatua na kuongeza ajira.

“Miaka ya nyuma sekta binafsi ilikuwa inachangia 30% lakini sasa inachangia 60% na Serikali 40% hii ni hatua ya kujivunia,”Mtendaji mkuu.

#NTTUpdates