×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

VIJANA WA ELIMU YA JUU NA DIMBWI LA DAWA ZA KULEVYA NCHINI.

Kwa mujibu wa Tafiti ndogo zilizo fanywa na jopo la Wataalamu wa udhibiti dawa zenye asili ya kulevya nchini zinaeleza kuwa asilimia kubwa ya Kundi la Vijana hususani wa Elimu ya juu,ndio wanaotajwa kujihusisha na matumizi ya Dawa zenye asili ya kulevya suala linalo hatarisha nguvu kazi ya Taifa.

Akiwa Jijini Arusha katika Kikao cha Kuweka Saini hati ya Ushirikiano (MoU) Kati ya Mamlaka za Udhibiti Kupitia DCEA na Sekta Binafsi Katika Kudhibiti Uchepushwaji wa Kemikali Bashirifu na Dawa Tiba Zenye Asili ya Kulevya, Kamishna Jenerali wa mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) Aretas Lyimo, anatumia jukwaa hilo kueleza Hali ilivyo katika sekta ya elimu na Vijana.

Kamishna Jenerali Lyimo, alisema kutokana na kuongezeka kwa tatizo la kutengeneza dawa za kulevya duniani ikiwemo utengezaji wa dawa mpya Kwa kutumia kemikali bashirifu na kushamiri kwa uchepushwaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya ambazo ni Fentanyl, Ketamine, Pethidine, Tramodol,na nyinginezo. Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwepo kwa wimbi kubwa la Vijana wanaotumia kemikali hizo na kuharibika kiafya na kiakili.

Alisema vijana wasomi wanatumia dawa za kulevya na kuharibika kiafya na kushindwa kupata watoto na huko mbeleni wanaweza kubaki wazee pekee na kusababisha ajira za wasomi kuchukuliwa na wageni kwasababu ya ukosefu wa vijana wasomi.

“Tumefanya utafiti mdogo na tumegundua vijana wasomi wanaongoza kwa matumizi ya dawa za kulevya na pia wengine wanasoma nchini Marekani na wengine vyuo vikuu hapa nchini na nchi nyinginezo, tutakosa wataalam wasomi badae sababu ya matumizi ya dawa tiba zenye asili ya madawa ya kulevya”

Alisema athari ya matumizi ya dawa hizi ni kubwa na mwisho wa siku wageni kutoka nje watashika nafasi hizi sababu hatuna wataalam katika fani nyinginezo sasa nawasihi nyie mnaouza kemikali muwe makini ili kudhibiti matumizi ya madawa haya.

#NTTUpdates