Na Mwandishi wetu
VIONGOZI wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Arusha wamempongeza mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa kumkabidhi Tuzo ya heshima kwa kazi nzuri anayofanya kwa wananchi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Ole Sabaya amesema kuwa tukio hilo la kukabidhi Tuzo hiyo ni heshima kwa kiongozi huyo kwa uongozi wake mahiri wa kuwajali wananchi hususani wa Mkoa wa Arusha.
“Tunaona kazi kubwa anayofanya Rais wetu maeneo mbalimbali ya nchi yetu,Arusha sasa hivi uchumi umerudi baada ya kusimama kipindi cha nyuma “amesema Ole Sabaya
Tuzo hiyo ya heshima ilitolewa katika sherehe za miaka 47 ya chama hicho tangu kuzaliwa kwake.