×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

VITAL’ O FC YAJIPELEKA MACHINJIONI

Na Mwandishi wetu.

MABINGWA wa ligi kuu Burundi Vital’O FC imehamishia mchezo wao wa nyumbani wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Young Africans SC, kwenye uwanja wa Azam Complex baada ya Burundi kukosa viwanja vyenye sifa na viwango vya CAF kuchezwa kwa mechi hizo.

Azam complex ambao ulikuwa ukitumiwa na Young Africans SC kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu msimu uliopita na hatua ya awali na raundi ya kwanza kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Young Africans SC wakiwa Azam complex hawajawahi kupoteza mchezo wowote huku wakiwa na historia ya kushusha vipigo vikubwa kwa wapinzani wao kwenye ikiaminika kama machinjio ya young Africans kwa wapinzani wao.

Vital’O FC ni kama wamejileta kwenye machinjio ya Wananchi ambayo wameyatumia kuwachinja wapinzani wao kwenye michuano mbalimbali .

Yanga imeendelea kupata bahati ya kuchezo michezo yote miwili hatua ya awali wakiwa nyumbani kama msimu uliopita dhidi ya ASAS ya Djibouti.

Mchezo wa kwanza Utachezwa Agosti 16-18 kwenye uwanja wa Azam Complex ampabo Vital’O FC watakuwa wenyeji na mchezo wa pili Utachezwa Benjamin Mkapa tarehe 23-25 Young Africans SC akiwa mwenyeji.

#NTTupdates