Na Mwandishi wetu.
Elimu ya msaada wa kisheria ya mama Samia imeendelea kutolewa kwa wananchi wa maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Arusha ambapo hii leo April 1, 2025 Wanasheria wa Kampeni hiyo wametoa elimu ya mirathi na wosia kwa wakazi wa Esilalei Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Wanufaika wa elimu hiyo kutoka katika jamii za kifugaji wameelezea namna ambayo elimu hiyo imewajengea uwezo wa kujua haki zao katika masuala ya kisheria na umuhimu wa utoaji wa wosia pamoja na ugawaji wa mali katika familia zao.
Elimu hiyo iliyotolewa kwa wananchi hao imejikita kwenye migogoro ya ardhi, familia, mirathi pamoja na migogoro ya kibiashara ambayo imekuwa ikiwakumba kwa kiasi kikubwa wananchi hao.
Ikumbukwe kuwa lengo la Kampeni hiyo ya msaada wa kisheria ya mama Samia ni kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani kufikia mwezi Mei 2025.
#NTTupdates.