Na Mwandishi wetu.
Watu wawili Oscar Emmanuel(20) mkazi wa mtaa wa Shadi kata ya Luchelele na Edwin Petro Bujuel(22) Mkulima na makazi wa mtaa wa Shadi kata ya Luchelele wauawa na Wananchi wenye hasira kali Kwa tuhuma za kumuua Dickson Madaraka Yusuph(24) kwa kumtenganisha kichwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali(Panga)
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza SACP Gedion Msuya.
Amesema chanzo cha Mauaji ya Kijana Dickson Madaraka Yusuph ni wivu wa kimapanzi kwani watuhumiwa hao walikua wanamtuhumu kua na mahusiano ya kimapenzi na Mke wa Oscar Emmanuel aitwaye Neema Joseph(17) mkazi wa mtaa wa shadi kata ya Luchelele .
Kwa mujibu wa taarifa ya kaimu Kamanda Msuya amesema kuwa tukio hilo la kuuawa kwa Dickson Madaraka Yusuph lilitokea mnamo Agosti 9, mwaka huu kandokando ya barabara Luchelele jijini Mwanza ambapo alikutwa ameuawa na kichwa chake kikiwa kimetenganishwa na kiwiliwili.
Aidha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ( SACP) Gideon Msuya amesema mara baada ya tukio la Mauaji ya kijana huyo jeshi la polisi kupitia msako mkali walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wawili ambapo kabla ya kupokea kipigo lutoka kwa eananchi ambao walikiri kuhusika na mauaji hayo.
Kamanda Msuya ameendelea kwa kusema watuhumiwa mara baada ya kukiri walikwenda kuonyesha mahali walipoficha kichwa cha marehemu pamoja na mali nyingine zingiwemo Pikipiki, yenye namba za usajiri MC 715 ENN aina ya TVS rangi nyeusi na simu ya mkononi aina ya Infinix Hot 10 ambazo zote ni mali za marehemu walizokuwa wamepora kabla na baada ya kutekeleza mauaji hayo.
Katika hali ya kusikitisha wakati wakiwa wanaonyesha mali za marehemu ndani ya msitu wa Nsumba wananachi wenye hasira kali walianza kuwashambulia watuhumiwa hao hadi kifo huku askari wa jeshi la polisi wakijeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao na kisha kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Kamanda msuya amesema miili ya marehemu hao imehifadhi Katika Chumba Cha kuhifadhia maiti kilichopo katika hospitali ya rufaa ya Kanda Bugando kwaajili ya kutambuliwa na kufanyiwa Uchunguzi Kutokana na tukio hilo.
Jeshi la Polisi limetoa Wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kujichukulia Sheria mkononi na jeshi Hilo halitosita kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu .
#NTTupdates