×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANAFUNZI TANDIKA SEKONDARI WAPEWA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.

WANAFUNZI wa kidato cha tatu na nne katika shule ya Sekondari Tandika iliyopo kata ya Tandika jijini Dar es Salaam wamepatiwa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ili wakawe mabalozi wazuri wa vitendo hivyo vya ukatili vinavyotokea kwa mabinti wa kike katika jamii.

Akizungumza katika semina hiyo mkufunzi wa mafunzo hayo Ahmed Kodi amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokea kwa mabinti wa kike vinasababishwa na ukosefu wa baadhi ya mahitaji.

Mafunzo hayo yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa UWT Temeke Comrade Lawama Mikidadi pamoja na Diwani wa viti maalum Mariam Mtemvu ambapo pamoja na mambo mengine wamewashika mkono wanafunzi wa kike kwa kwa kuwapatia taulo za kike.

“Tumekuja hapa kuwaletea taulo za kike ambazo zitawasaidia wakati wa hedhi kwani limekuwa tatizo kubwa hasa kwa wasichana hasa wanafunzi, lakini elimu hii ya kupinga ukatili wa kijinsia mtakayoipata hapa muilewe vizuri ili mkawe mabalozi katika jamii zetu” amesema Hata hivyo Mtemvu pamoja na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Temeke Lawama Mikidadi walipata wasaa wa kwenda katika Hospital ya Sandali na kukutana na wamama waliojifungua na wajawazito na kuzungumza nao kuhusu lishe na malezi kwa watoto pamoja na kugawa pempasi kwa wazazi kwaajili ya watoto waliozaliwa.

#NttUpdates.