×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANAFUNZI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOWEKWA SHULENI

Na Mwandishi wetu.

Wanafunzi watakiwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizowekwa shuleni ili kupata haki zao na kutimiza wajibu wao kama ilivyoanishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Na Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THUBU) wakati wa kutoa elimu ya haki za mtoto na ukatili dhidi ya watoto katika Shule ya Sekondari ya Margreth sitta iliyopo wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Mohamed amesema kuwa kutokana na kuendelea kwa utandawazi kumekuwa na mwenendo mbaya wa mmomonyoko wa maadili kwa Wanafunzi hali ambayo husababisha kuvunjwa kwa haki zao za msingi kama vile haki ya kupata elimu.

“Wanafunzi wanaingia katika makundi yasiyofaa matokeo yake wanapata mimba na kusababisha kuacha shule” amesema Mohamed

Kwa upande wake Veronica Goodluck, askari Polisi kutoka dawati la Jinsia na watoto katika Kituo cha (W) Urambo alitoa wito kwa wanafunzi hao kueza kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao.”Yote yanaezekana kwakujiepusha kuingia katika makundi yasiyofaa” amesema Bi. Veronica

Naye, Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu anayeitwa Mbombilie Elias Shiloti ameishukuru THBUB kwakutoa elimu kwa wanafunzi hao kwani kufanya hivo imeweza kusaidia wanafunzi hao kuweza kutambua haki na wajibu wao.

#NTTupdates