Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda leo Aprili 15, 2025 amefanya ziara mahususi kwaajili ya kuwasikiliza wananchi wa mtaa wa Longdon-Mazengo Kata ya Sokoni One ambao wamekuwa wakilalamikia kuhusu ubovu wa kivuko kilichopo katika mtaa huo huku akiahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea na jitahada mbalimbali za kuhakikisha kuwa miundombinu ya mkoa wa Arusha inakuwa imara nyakati zote.
Makonda amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kutunza na kudumisha amani na utulivu ndani ya mkoa akiwataka kufuata utaratibu pale panapotokea migogoro au sintofahamu za kiutendaji kwenye maeneo yao.
Aidha, Makonda amewahimizi wananchi hao juu ya umuhimu wa kuhudhuria vikao mbalimbali vinavyoitishwa na viongozi wa maeneo yao ili kujua mipango na malengo ya maendeleo katika maeneo yao sambamba na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili.
#NTTupdates.