×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU YA KUKOMESHA UVUVI HARAMU

Na Mwandishi wetu.

Wananchi wa Mkoa wa Mwanza wameiomba serikali kutoa elimu Stahiki kwa wavuvi kuhusu masuala ya uvuvi haramu, ili kusaidia kupunguza wimbi na upotevu wa vizalia vya mazao ya samaki katika ziwa Viktoria.

Wananchi hao wamesema, mpaka sasa bado wapo wavuvi ambao hawafahamu athari za uvuvi haramu hali ambayo inafanya waendelee kujihusisha na uvuvi huo ambao kwa kiasi kikubwa unaathiri mazalia ya samaki na kusababishwa upotevu mkubwa wa mazalia hayo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema ili kupambana na uvuvi haramu serikali imeendelea kufanya doria katika ziwa na tayari imeshanunua ndege nyuki (drone) ambayo itatumika kufanya doria katika ziwa Viktoria.

Amesema drone hiyo itakuwa ikifatilia mwenendo wa uvuvi katika ziwa Victoria ili kutokomeza kabisa shughuli aramu ambazo zimekuwa zikifanywa na wavuvi wasio waaminifu na zoezi Hilo litakuwa endelevu.

#NTTUpdates