×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI WAIRARUA TABORA UNITED 3-0

Na Mwandishi wetu.

Dakika 90 zimemalizika kwenye dimba la Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora na kushuhudia Wananchi Young Africans SC wakitakata baada ya kuwatandika Tabora United magoli 3 -0 na kulipa kisasi chao.

Magoli ya Young Africans SC yamefungwa na mlinzi Israh mwenda dakika ya 21, mshambuliaji Clement Mzize dakika ya 57 na goli la tatu likifungwa na mshambuliaji Prince Dube dakika ya 68 na kupeleka furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Mchezo huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili hasa baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa Tabora United kuitandika Young Africans SC magoli 3 -1 kwenye dimba la Azam Complex na waikiahidiwa kitita cha Milioni 60 kama wangefanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo.

#NTTupdates