Na Mwandishi wetu.
Dakika 90 zimemalizika kwenye mchezo wa mwisho wa ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) uliowakutanisha Wananchi Young Africans SC dhidi ya MC Alger na mchezo huo kuisha kwa Suluhu ya bila kufungana.
Young Africans SC, walitakiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kufuzu robo fainali lakini mambo yakawa magumu upande wao na kulazimishwa sare kwenye mchezo huo.
#NTTupdates