×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WANANCHI WATENGENEZA BARABARA KWA NGUVU ZAO.

WAKAZI wa Mtaa wa Masemele Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza, wamejitokeza kutengeneza barabara katika mtaa wao ili kuboresha miundombinu ya barabara iliyoharibika.

Aidha muitikio huo unakuja kufuatia adha kubwa ya ubovu wa barabara hasa katika msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha, hivyo wamesema wameamua kutengeneza barabara hiyo ili iweze kupitika na kupata baadhi ya huduma za kijamii.

Mwenyekiti wa mtaa huo Yohana Mashamba amesema wametengeneza barabara hiyo kwa nguvu zao na kuomba Serikali iwasaidie kurekebisha miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika hasa katika msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha.

#NTTUpdates