×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WASIRA AWASILI MARA, KUSAKA KURA ZA DKT. SAMIA, NA KUWANADI WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

Na Mwandishi wetu.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amewasili mkoani Mara kwa ziara ya kuwanadi wagombea ubunge, udiwani na kumwombea kura mgombea urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Baada ya kuwasili, Wasira alishiriki kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mara na kufuatiwa na kikao cha ndani wilayani Butiama ambako pamoja na mambo mengine aliwasihi wana CCM kumpigia kura mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama, Dk. Wilson Mahera na kumwombea kwa kura za kishindo yeye na Dk. Samia kwa wananchi.

Aidha, Wasira alizuru kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wilayani Butiama.

Akiwa Musoma mjini, Wasira atahutubia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Mkendo na kumwombea kura Dk. Samia, wagombea ubunge na udiwani wa mkoa huo.

#NTTupdates