Na Mwandishi wetu.
Wataalamu na Wakuu wa vituo vya Afya na Zahanati Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara, wamepatiwa mafunzo ya Mpango wa Afya wa (CCHP) kupitia mfumo wa PLANREP( planning and Reporting).
Mafunzo hayo ya mfumo wa PLANREP, yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati kwa lengo la kuwawezesha Wataalamu hao kuandaa Bajeti inayokidhi vigezo katika vituo vya Afya pamoja na utoaji wa ripoti ya utoaji wa huduma katika kila kituo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa DKt. Pastory Mahendeka amewataka Wataalamu hao kuwa makini ili waweze kuuelewa mfumo huo vizuri kwani ndiyo msingi wa utekelezaji wa shughuli za Afya.
#NTTupdates