Kwa mujibu wa Chama cha Madaktari cha Kenya, Polisi katika mji mkuu wa Nairobi, wanadaiwa kuwauwa kwa kuwapiga risasi watu watano walipokuwa kwenye maandamano makubwa yaliofanyika, kupinga Muswada wa fedha 2024 uliopanga kupita kwa mwaka huu 2024.
Mapema Jana mchana kundi la waandamanaji ilivuka mstari wa ulinzi wa polisi na kuingia bungeni, kufanya uharibifu mkuvwa ikiwa ni pamoja na kuwasha moto katika sehemu ya eneo hilo.Moto huo pia ulizuka katika Ukumbi wa Jiji la Nairobi,makao makuu ya kaunti hiyo.
Takriban watu 40 wanaendelea kupatiwa hospitalini.
#Nttupdates