×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

WATUMISHI WIZARA YA UJENZI WAKUMBUSHWA WAJIBU WAO KATIKA JAMII

Na Mwandishi wetu.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Jacob Rombo amewataka watumishi wa Wizara ya Ujenzi kuzingatia maadili na kanuni katika kazi zao pamoja na miongozo na taratibu iliyowekwa na Serikali katika utimizaji wa majukumu hayo.

Rombo amesema hayo leo Julai 01, 2025 mkoani Arusha wakati akifungua mafunzo ya huduma kwa mteja katika mazingira ya utendaji kazi katika utumishi wa umma yanayotolewa na Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yanayofanyika mkoani humo.

Amesisitiza umuhimu wa mafunzo hayo ya kiutendaji ya utumishi wa umma ya mara kwa mara kwa ajili ya kuendelea kuwafundisha na kuwakumbusha watumishi hao wajibu wao wanaopaswa kufanya katika jamii.

Katika hatua nyingine, Rombo amepongeza Uongozi wa Wizara ya Ujenzi kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja mbalimbali iliyokamilika na ile inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa huo na mikoa mingine ya Tanzania kwani kwa kukamilika kwake inaleta tija kwa wananchi katika ufanyaji wa shughuli zao za kila siku.

#NTTupdates.