Na Mwandishi wetu.
Jeshi la Polisi nchini limetolea ufafanuzi tukio linalosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ikionyesha kijana aliyefingwa Mikono huku akipigwa kwa fimbo.
Katika Taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la polisi, imeeleza kuwa tukio hilo limetokea Juni 26, Mwaka huu na kutokana na kushambuliwa Kwa kijana huyo anayejulikana Kwa jina la Enock Thomas Mhangwa alifariki Dunia.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Jeshi la Polisi Mkoani Geita limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuhusika Katika mauaji hayo, ambao ni Ferdinand Antony Masembo Afisa Mtendaji wa Kijiji Cha Liyobahika na Hussein Ally Madebe.
Msemaji wa Jeshi hilo Amesema kuwa Watuhumiwa Wengine wanaendelea kutafutwa akiwemo Mtendaji wa Kijiji Cha uyovu na Mgambo wawili ambao wamekimbia.
Jeshi la Polisi limewatahadharisha watu wenye tabia ya kujichukulia Sheria mkononi, Kuacha mara Moja tabia hizo kabla Sheria haijafuata mkondo wake dhidi Yao.
#NTTUpdates