Na Mwandishi wetu
Habari njema kwa mashabiki wa Manchester City baada ya kurejea na kuanza mazoezi kwa wachezaji muhimu wa kikosi hicho, ambao walikosekana kwenye michezo kadhaa na kushuhudia Man City ikichezea vichapo michezo minne mfululizo.
Nyota ambao wameanza mazoezi kwenye kikosi hicho ni Kevin De Bruyne (33) ambae amecheza michezo 8, akifunga goli 1 na assist 1 kabla ya kupata majeraha.
Wachezaji wengine ni Mlinzi wa kati John Stone (30) raia wa Uingereza, Manuel Obafemi Akanji (29) mlinzi wa kati pamoja na kiungo mshambuliaji Jack Grealish (29).
Kurejea kwa wachezaji hao kumepelekea matumaini mapya kwa Kocha Pep Guardiola kurejea kwa kasi mpya kusaka taji la EPL.
#NTTupates